Maswali yaliyojibwa na WHO kuhusu COVID-19

Home/Corona Virus/Maswali yaliyojibwa na WHO kuhusu COVID-19
Je! Kirusi cha korona ni nini?2020-03-26T07:56:02+03:00

Kirusi cha korona ni familia kubwa ya virusi ambayo vinaweza kusababisha magonjwa kwa wanyama au binadamu. Kwa binadamu, ugonjwa wa kirusi cha korona kadharika kusababisha magonjwa ya kupumua yanayoanza na homa ya kawaida kwenda magonjwa mabaya kama vile Middle East Respiratory Syndrome (MERS) na Severe Acute Respiratory Syndrome (SARS). Kirusi cha korona kilichotambuliwa hivi karibuni husababisha ugonjwa wa COVID-19.

COVID-19 ni nini?2020-03-26T08:15:57+03:00

Ni ugonjwa wa kuambukiza unaosababishwa na kirusi cha korona kilichoguliwa kirusi cha korona kilichogundulika hivi karibuni. Kirusi hiki kipya na ugonjwa haukujulikana hapo mwanzo kabla ya mlipuko kuanza huko Wuhan nchini China, mnamo Disemba 2019

Je! COVID-19 ni sawa na SARS?2020-03-26T08:18:15+03:00

Hapana. Virusi vinavyosababisha COVID-19 na vile vilivyosababisha mlipuko wa SARS mwaka 2003 vinahusiana kwa vinasaba, lakini magonjwa yanayosabishwa ni tofauti kidogo. SARS ulikua na vifo vingi lakini hali ya maambukizi ni kidogo kuliko COVID-19. Hakujatokea mlipuko wowote wa SARS duniani tangu mwaka 2003.

Nini Dalili za COVID-19?2020-03-26T08:22:06+03:00

Dalili za kawaida za ugonjwa wa COVID-19 ni:

  1. Homa
  2. Uchovu
  3. Kikohozi kikavu.
  • Baadhi ya wagonjwa wanaweza kupata maumivu, msuguano wa pua, kutokwa kwa majimaji puani, vodonda vya koo au kuharisha.
  • Dalili hizi huanza polepole. Baadhi ya watu wanapata maambukizi bila kuonesha dalili zozote za ugonjwa.
  • Watu wengi (takribani 80%) wanapona kutokana na ugonjwa huu bila ya matibabu maalum. Takribani katika kila watu 6 wenye ugonjwa wa COVID-19 mtu 1 huwa mgonjwa sana na kupelekea kupumua kwa shida.
  • Wazee na wale wenye shida za kimatibabu kama vile shinikizo la damu, matatizo ya moyo au ugonjwa wa kisukari wana uwezekano wa kupata ugonjwa kwa dalili mbaya.
  • Watu wenye homa, kikohozi na ugumu wa kupumua wanapaswa kupata matibabu.
Ugonjwa wa COVID-19 unaenea vipi?2020-03-26T08:27:23+03:00

Mtu anaweza kupata ugonjwa wa COVID-19 kutoka kwa watu wenye kirusi.

Ugonjwa unaweza kuenea kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine kupitia matone madogo kutoka puani au mdomoni mwa mgonjwa wa COVID-19 anapokohoa au kutoa hewa.

Matone haya hutua kwenye vifaa/vitu na maeneo yanayomzunguka binadamu.

Watu wengine hupata ugonjwa wa COVID-19 kwa kugusa vitu hivi, kisha kujigusa machoni, puani au mdomoni.

Pia mtu anaweza kupata COVID-19 ikiwa anavuta matone kutoka kwa mtu aliye na COVID-19 anayekohoa au kutoa hewa nje. Hii ndio sababu ni muhimu kukaa mbali na mtu ambaye ni mgonjwa zaidi ya mita 1 (miguu 3).

WHO ikiwa inakagua utafiti unaoendelea juu ya njia ambazo COVID-19 imeenea na itaendelea kutoa matokeo mapya.

Je! Kirusi cha COVID-19 kinaweza kusambazwa kwa njia ya hewa?2020-03-26T08:28:41+03:00

Hadi sasa uchunguzi unaonyesha kuwa virusi vinavyosababisha COVID-19 husambazwa kwa njia ya kugusana kwa matone ya kupumua kuliko kwa njia hewa.

Je! COVID-19 inaweza kupatikana kwa mtu ambaye hana dalili?2020-03-26T08:29:44+03:00

Njia kuu ambayo ugonjwa huenea ni kupitia kuvuta matone kutoka kwa mtu anayekohoa. Hatari ya kushika COVID-19 kutoka kwa mtu ambaye hana dalili hata kidogo ni ndogo sana. Walakini, watu wengi walio na COVID-19 wanapata dalili kali tu. Hii ni kweli hasa katika hatua za mwanzo za ugonjwa. Kwa hiyo inawezekana kupata COVID-19 kutoka kwa mtu ambaye ana dalili, kwa mfano, kikohozi kidogo tu na hajisikii mgonjwa.

Naweza kupata COVID-19 kutoka kwenye kinyesi cha mtu aliye na ugonjwa?2020-03-26T08:31:52+03:00

Hatari ya kupata COVID-19 kutoka kwenye kinyesi cha mtu aliyeambukizwa inaonekana kuwa ndogo. Wakati uchunguzi wa awali unaonyesha virusi vinaweza kuwapo kwenye kinyesi katika visa vingine, kuenea kwa njia hii sio sababu kuu ya mlipuko.

WHO inakagua utafiti unaoendelea juu ya njia ambazo COVID-19 imeenea na itaendelea kutoa matokeo mapya. Sababu hii ni hatari, hata hivyo, ni sababu nyingine ya kusafisha mikono mara kwa mara, baada ya kutoka chooni na kabla ya kula

Je! Binadamu wanaweza kuambukizwa COVID-19 kutoka kwa mnyama?2020-03-26T08:34:42+03:00

Virusi vya korona ni familia kubwa ya virusi ambayo ni vya kawaida katika wanyama. Wakati mwingine, watu huambukizwa na virusi hivi ambavyo vinaweza kuenea kwa watu wengine. Kwa mfano, SARS-CoV ilihusishwa na paka na MERS-CoV husambazwa na ngamia. Uwezekano wa wanyama kuwa chanzo cha COVID-19 bado haujathibitishwa

Ili kujikinga, kama vile wakati wa kutembelea masoko ya wanyama hai, epuka kugusana moja kwa moja na wanyama pamoja na mazingira yao. Hakikisha mazoea mazuri ya usalama wa chakula wakati wote. Hifadhi nyama mbichi, maziwa au sehemu za wanyama kwa uangalifu ili kuzuia uchafuzi wa vyakula visivyopikwa na epuka kula bidhaa mbichi za wanyama au ambazo hazijaiva vizuri katika kupikwa.

Je! Ninaweza kupata COVID-19 kutoka kwa mnyama ninayemfuga?2020-03-26T08:35:29+03:00

Hakuna ushahidi kwamba mbwa, paka au mnyama yeyote afugwaye anaweza kusambaza COVID-19. COVID-19 inasambazwa zaidi kupitia matone yanayotokana na mtu mwenye maambukizi iwapo anakohoa, piga chafya au kuzungumza. Ili kujilinda safisha vizuri mikono yako mara kwa mara.

Virusi hukaa kwenye nyuso za vitu kwa muda gani?2020-03-26T08:37:23+03:00

Haijafahamika kwa muda gani virusi vinavyosababisha COVID-19 hukaa kwenye eneo husika, lakini inaonekana kuwa na tabia kama za virusi vingine. Uchunguzi unaonyesha kuwa virusi vya korona (pamoja na maelezo ya awali juu ya virusi vya COVID-19) vinaweza kuendelea kuwepo kwenye nyuso za vitu husika kwa masaa machache au hadi siku kadhaa. Hii inaweza kutofautiana kutokana na hali tofauti (kama, aina ya eneo,joto au unyevu wa mazingira).

Ikiwa unafikiri eneo husika linaweza kuwa na maambukizi, safisha na dawa ya kuua virusi ili kujilinda wewe na wengine. Osha mikono yako na kwa kutumia vitakasa au kwa maji na sabuni. Epuka kujigusa macho, mdomo, au pua

Je! Ni salama kupokea mzigo kutoka eneo lolote ambalo maambukizi ya COVID-19 yameripotiwa?2020-03-26T08:38:12+03:00

Ndio. Uwezo wa mtu aliyeambukizwa kusambaza ugonjwa kwenye bidhaa za kibiashara ni mdogo na hatari ya virusi vinavyosababisha COVID-19 kukaa kwenye mzigo/kifurushi ambacho kimehamishwa, kusafiri, na kuwekwa katika hali joto tofauti ni mdogo pia.

Hatua za kujilinda kwa kila mtu2020-03-26T08:49:08+03:00

1. Zingatia habari za hivi karibuni juu ya milipuko ya COVID-19, inayopatikana kwenye Shirika la Afya Duniani (WHO) na kupitia mamlaka yako ya kitaifa ya afya. Nchi nyingi duniani kote zimesharipoti kesi za milipuko ya COVID-19. Nchini China na baadhi ya nchi zingine zimefanikiwa kupunguza au kuzuia milipuko yao. Walakini, hali hiyo haitabiriki hivyo tembelelea mara kwa mara kwa habari mpya zaidi. Unaweza kupunguza nafasi ya kuambukizwa au kueneza COVID-19 kwa kuchukua tahadhari rahisi

2. Safisha mikono yako mara kwa mara kwa kutumia vitakasa au osha kwa sabuni na maji.

Kwanini? – Kuosha mikono yako kwa sabuni na maji au kutumia vitakasa huua virusi ambavyo vinaweza kuwepo mikononi mwako

3. Kaa umbali wa angalau mita 1 (miguu 3) kati yako na mtu yeyote anayekohoa au kupiga chafya.

Kwa nini? Wakati mtu anakohoa au kupiga chafya hunyunyiza matone ya kioevu kutoka puani au mdomoni ambayo yanaweza kuwa na virusi. Ikiwa upo karibu naye Zaidi, unaweza kuvuta matone pamoja na virusi vya COVID-19 ikiwa mtu anayekohoa ana ugonjwa.

4. Epuka kugusa macho, pua na mdomo

Kwa nini? Mikono hugusa sehemu mbalimbali na inaweza kuchukua virusi. Mara ikichukua virusi, inaweza kupeleka virusi hivyo kwenye macho yako, pua au mdomo. Baada ya hapo, virusi vinaweza kuingia ndani ya mwili wako na vinaweza kukufanya uwe mgonjwa.

5. Hakikisha wewe, pamoja na watu wanaokuzunguka, mnafuata usafi mzuri wa kupumua. Hii inamaanisha kufunika mdomo wako na pua kwa kiwiko cha mkono wako au tishu wakati unapokohoa au kupiga chafya. Kisha tupa tishu zilizotumika mara moja.

Kwa nini? Matone hueneza virusi. Kwa kufuata usafi mzuri wa kupumua unalinda watu wanaokuzunguka kujilinda na virusi kama vile homa, mafua na COVID-19

6. Kaa nyumbani ikiwa unajisikia vibaya. Ikiwa una homa, kukohoa na kupumua kwa shida,pigi simu mapema ili kupata matibabu. Fuata maagizo ya mamlaka ya afya ya eneo lako.

Kwa nini? Mamlaka ya kitaifa na ya ndani zinapata habari mpya kuhusu haliya sasa katika eneo lako. Kupigia simu mapema itaruhusu mtoaji wako wa huduma ya afya kukuelekeza haraka katika kituo cha afya kinachofaa. Hii pia itakulinda na kusaidia kuzuia kuenea kwa virusi na maambukizi mengine.

7. Fuatilia habari mpya za hivi karibuni za COVID-19 (miji au maeneo ya ndani ambayo COVID-19 inaenea sana). Ikiwezekana, epuka kusafiri kwenda maeneo – haswa ikiwa wewe ni mzee au una ugonjwa wa kisukari, moyo au mapafu.

Kwa nini? Una nafasi ya juu ya kupata maambukizi ya COVID-19 katika moja ya maeneo haya.

Nifanye nini kama nilitembelea eneo ambalo COVID-19 imesambaa?2020-03-26T08:55:29+03:00

Kama hivi karibuni ( siku 14 zilizopita) umetembelea maeneo ambayo COVID-19 imesambaa, fuata muongozo uliotolewa kwenye swali la 15. ( Nini naweza kufanya ili kujikinga na kuzuia maambukizi?) kisha fanya yafuatayo:

  1. Jitenge kwa kukaa nyumbani mpaka upone hii ni kama umeanza kutojisikia vizuri,hata kama dalili ni za kiasi kama kichwa kuuma, homa ya chini ( nyuzi joto 37.3 C au zaidi ) na kuvuja kwa pua.
  2. Kama inawezekana kuwa na mtu wa kukuletea mahitaji yako au ukitoka nje kununua chakula, basi vaa barakoa ( mask) kuzuia kuwaambukiza wengine. Kwanini? – Kuzuia kukutana na watu wengine na kwenda katika vituo vya afya vitafanya vituo hivi kufanya kazi kwa ufanisi na kuwasaidia kujilinda mwenyewe na wengine dhidi ya COVID-19 na virusi vingine.
  3. Ukipata homa, kikohozi na shida ya kupumua, fata ushauri wa kiafya zaidi inawezekana kuwa na maambukizi kwenye njia ya hewa au matatizo mengine makubwa zaidi. Piga simu na kuwajulisha watoa huduma ya afya juu ya safari zako za karibuni au mkutaniko na wasafiri.  Kwanini? – Kupiga simu hii itawasaidia watoa huduma kukuelekeza kituo sahihi cha afya karibu na wewe. Hii pia huzuia kusambaza COVID-19 na virusi vingine.
Kuna matibabu gani ya COVID-19 ( ikiwemo vidonge, chanjo, na tiba mbadala)?2020-03-26T08:59:34+03:00

Je Antibiotiki ( vijiuasumu) vinaweza kuzuia au kutibu COVID-19?

Hapana. Antibiotiki hazifanji kazi dhidi ya virusi,hufanya kazi ya kuuwa bakteria pekee.COVID-19 inasababishwa na kirusi, kwahiyo antibiotiki hazitafanya kazi. Hazifai kutumika kama njia ya kujikinga au kutibu COVID-19. Zitumike pale tu endapo daktari atashauri kutibu maambukizi ya bakteria.

Je kuna dawa nyingine au tiba mbadala zinazozuia COVID-19?

Wakati tiba za maghalibi, asili na za nyumbani zinaweza kuleta auheni ya dalili za COVID-19, hakuna ushahidi wahivi karibuni wa dawa zozote zinazoweza kuzuia au kutibu hili gonjwa. WHO haipendekezi tiba binafsi kwa kutumia dawa yoyote, ikiwemo antibiotiki,kama kinga na tiba ya COVID-19. Hata hivyo , kuna majaribio yanafanywa yanayotumia kuchanganya tiba asili na zile za magharibi. WHO itaendelea kutoa mrejesho wa taarifa pale punde tiba itakapo gundulika.

Kuna chanjo, dawa au tiba ya COVID-19?

Mpaka wa leo bado hakuna chanjo na dawa za kuuwa virusi inayozuia COVID-19. Japo kuwa, wale walioathirika wanapaswa kupewa uangalizi ili kupunguza dalili. Watu wenye magonjwa sugu wanapaswa kulazwa hospitali. Wagonjwa wengi wanapata ahueni kutokana na uangalizi wanaopatiwa.

Chanjo za majaribio na dawa maalumu bado zipo chini ya uchunguzi. Zimekuwa zikitumiwa kwa majaribio ya kliniki.WHO inaratibu juhudi za kutengeneza chanjo na madawa kuzuia na kutibu COVID-19.

Njia madhubuti kujikinga binafi na wengine dhidi ya COVID-19 ni kuosha mikono mara kwa mara, kujifunika kwa kiwiko au kitambaa wakati unapokohoa, na kuweka umbali wa japo mita 1 ( futi 3) na watu wanaokohoa au kupiga chafya.

Je nivae barakoa ili kujilinda?2020-03-26T09:01:00+03:00

Vaa barakoa kama unaumwa na dalili za COVID-19 ( hasa kikohozi) au kama unamuuguza mtu alieathirika na COVID-19.Barakoa za kutumia na kutupa zinafaa kutumika mara moja tu. Kama auhumwi au kuuguza mgonjwa basi unatumia barakoa vibaya. Kuna uhaba wa barakoa ulimwenguni, hivyo WHO inaomba zitumike kwa busara.

WHO inashauri kutumia barakoa za kiafya kuzuia matumizi yasiyo ya lazima ya rasilimali na matumizi mabaya ya barakoa.

Njia pekee ya kujilinda mwenyewe na wengine dhidi ya COVID-19 ni kuosha mikono, kufunika kwa kiwiko au kitambaa wakati unapokohoa au kupiga chafya.

Kukabiliana na msongo wakati wa COVID-192020-03-26T14:23:24+03:00
  • Ni kawaida kuwa na huzuni, sonona, kuchanganyikiwa, kuogopa au hasira wakati wa majanga. Kuongea na watu unaowaamini husaidia. Wasiliana na marafiki na familia.
  • Kama utakaa nyumbani, dumisha mfumo wa maisha wenye afya- ikiwemo mlo bora, kulala, mazoezi na mawasiliano ya kijamii na uwapendao nyumbani na barua pepe au simu kwa familia na marafiki.
  • Usivute sigara, pombe au vilevi vingine katika kukabili hali hisia zako. Kama unahisi kuzidiwa zaidi, ongea na mtu wa afya au mshauli. Ikiwezekana weka mipango,wapi pakwenda na jinsi ya kupata huduma ya afya ya mwili na akili.
  • Pata ukweli.Kusanja taarifa ambazo zitakusaidia kwa ufasaha kujua hatari ili uweze kuchukua hatua zinazofaa, Tafuta chanzo kinachoaminika kama tovuti ya shirika la afya duniani WHO , au la ndani au shirika la afya kitaifa.
  • Zuia wasi na mvutano kwa kupunguza muda wa wewe na familia yako kuangalia au kusikiliza vyombo vya habari ambavyo unaona vinaleta huzuni.
  • Tumia ujuzi ambao umeshautumia kitambo ambao umekusaidia kupambana na magumu ya maisha na utumie ujuzi huo kukusaidia kuthibiti hisia zako katika kipindi hiki cha mlipuko wa ugonjwa.

Kuwasaidia watoto katika kukabiliana na msongo wakati wa COVID-19

  • Watoto huonyesha msongo kwa njia tofauti kama vile kuwa na mashaka, kujiondoa, hasira au mvutano, kujikojolea n.k. Itikia matendo ya mwanao kwa njia chanya, sikiliza mahitaji yao na wape upendo na umakini zaidi.
  • Watoto wanahitaji upendo kwa watu wazima kipindi hiki kigumu. Wapatie muda na umakini wako zaidi. Kumbuka kuwasikiliza, kuongea kwa upole na kuwahakikishia. Ikiwezekana, tengeneza mazingira waweze kucheza na kupumzika.
  • Jaribu kuwaweka watoto karibu na wazazi na familia na acha kuwatenga mbali watoto na walezi wao. Kama utengano ukitokea (mf. Kulazwa) hakikisha kuna mawasiliano endelevu ( simu) na wape uhakika.
  • Endeleza ratiba na njia zile zile iwezekanavyo, au saidia kutengeneza mpya katika mazingira mapya, ikiwemo shule/kujifunza na kucheza katika hali ya usalama.
  • Toa ukweli kuhusu kinachoendelea, elezea kinachoendelea na wapatie taarifa sahihi ya jinsi ya kupunguza hatari ya maambukizi kupitia maneno watakayo weza kukuelewa kutokana na umri wao. Hii pia inajumlisha kuwapa taarifa kuhusu matarajio ya mbeleni (kama mmoja wa familia ataumwa na atahitaji kwenda hospitali.
2020-11-30T14:10:31+03:00
Go to Top